re

Friday, April 6, 2012

R.I.P STEVEN KANUMBA a.k.a KANUMBA THE GREAT


Habari zilizotufikia hivi sasa zinasema msanii maarufu nchini, Steven Kanumba amefariki dunia ghafla baada ya kudondoka na kujingonga sehemu ya kisogo akiwa nyumbani kwake Vatican, Sinza jijini Dar es Salaam. Tukio hilo limetokea majira ya saa 7 usiku wa kuamkia leo na taarifa za kudondoka kwa Kanumba zilitolewa na kijana anayeishi nae hapo nyumbani ajulikanaye kwa jina la Seti aliyemwita daktari kujaribu kuokoa maisha yake lakini alipofikishwa hospitali ya Muhimbili tayari alikuwa amekata roho. Kwa sasa mwili wa marehemu umeifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Taifa Muhimbili. Habari zaidi zitawajia baadae.

KILICHOMUUA MAREHEMU STEVEN KANUMBA a.k.a THE GREAT HIKI HAPA

KWA MUJIBU WA MSAIDIZI  WA MAREHEMU STEVE KANUMBA, (BWANA SETI) ALISEMA KUWA ELIZABETH MICHAEL  MAARUFU KAMA LULU ALIKUJA NYUMBANI KUKAWA NA KAUGOMVI AMBAPO WAKAINGIA CHUMMBANI WAKIWA HUKO BAADA YA MUDA,LULU ALITOKA NA KUMUITA YEYE  KUMUAMBIA KANUMBA KAANGUKA, YE ALIPOENDA AKAMKUTA KAANGUKA NDIO AKAENDA MUITA DAKTARI WA KANUMBA AMBAPO ALIPORUDI HAKUMKUTA LULU, LAKINI  HADI TUNAVYOONGEA LULU YUKO POLISI OSTERBAY KWA AJILI YA MAHOJIANO NA POLISI

Inasemekana Lulu aligombana na marehemu Kanumba ambaye inasemekana alikuwa mpenzi wake baada ya kukutwa akiongea na mwanaume mwingine,kwenye simu au live mimi sijui- kitendo ambacho kilimuudhi marehemu.. Lulu anasemekana kumsukuma marehemu na ndipo alianguka na umauti kumfikia jana usiku...credit to www.kabelelejr.blogspot.com  (Seif Kabelele)

No comments:

Post a Comment