Msanii maarufu wa filamu hapa
nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ leo amepandishwa kizimbani katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa
shitaka la mauaji.
Lulu
alipandishwa kizimbani kwa usiri mkubwa akitokea Kituo cha Polisi cha
Oysterbay alikokuwa akishikiliwa na kupandishwa kizimbani moja kwa moja
bila kuwekwa mahabusu ya mahakama hiyo kama iwavyo kwa washitakiwa
wengine wanaosubiri kusomewa kesi zao.
Baada
ya kupandishwa kizambani alisomewa shitaka lake na Mwendesha Mashtaka
Mkuu wa Mahakama hiyo, Elizabeth Kaganda ambapo alisema Mnamo Aprili 7
mwaka huu majira ya saa saba za usiku maeneo ya Sinza Vatican jijini Dar
es Salaam Elizabeth Michael (18) alimuua Steven Kanumba. Katika kesi
hiyo mshitakiwa hakutakiwa kujibu lolote isipokuwa alinyoosha kidole na
kupinga umri uliotajwa kuwa ana miaka 18 na kusema umri wake ni miaka
17. Baada ya kusomewa shitaka hilo, Lulu alipelekwa gerezani Segerea na
kesi yake itasikilizwa tena aprili 23 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment